Jumanne, 15 Aprili 2014
WANAUME NA MITINDO YA NYWELE.
Habari za asubuhi wapendwa wasomaji wa blog hii natumaini tupo wazima tumshukuru Mungu kwa yote na tuwaombee wale walio athirika na mafuriko waweze kupato sehemu ya kuishi na waendelea na shughuli zao.
Siku ya leo nitazungumzia kuhusu Mtindo ya Nywele kwa wanaume inavyoweza kumfanya mtu aonekane tofauti, Kuna aina mbali mbali ya mtindo ya nywele kwa wanaume kuna wanaume wanapenda kunyoa mitindo mbali mbali ya nywele na kuna wengine wanapenda kusuka mitindo mbali mbali.
Hizi ni baadhi ya mitindo mbali mbali ya nywele:

Mtindo huu unapendwa na wanaume wanaopenda kusuka aina tofauti tofauti za nywele.Sio wanaume wote wanapenda kusuka nywele,ila wanaume wengine wanapenda sana kusuka mitindo mbali mbali ya nywele na moja wapo ni huo mtindo hapo juu.

Moja wapo ya mtindo wa nywele unaopendwa sana na wanaume wengi sana wanapenda kunyoa style hii ya nywele ambayo inaitwa kama ( kiduku) ni style ambayo haiwezi kuisha fashion kuliko style nyingine za nywele.

Style nyingine ya nywele kwa wanaume ambao wanapenda kusuka nywele zao kwa kuchanganya na lasta na kuweka vishanga kwenye nywele zao, kama unavyoona kwenye picha hapo juu.
WANAUME NAO HATUWASAHAU KATIKA KUPENDEZA NA VITENGE
Siku ya leo nitazungumzia kuhusu vazi la kitenge kwa Wanaume kuonekana tofauti na wenye kuvutia mda wote. Vazi la kitenge kwa wanaume linaweza kushonwa kama suti na mtindo mbali mbali.
Hizi ni baadhi ya picha za wanaume wakiwa wamevaa suti za kitenge.
Hili ni moja wapo ya vazi la kitenge muundo wa suti.
Sio wanaume wote vakivaa vazi hili wanavutia unatakiwa kwa kuangalia umbo lako kwanza sio umemuona mtu amevaa na we unaenda kushona vazi kama hili.
Tukiangalia hizo picha hapo juu imeonesha models wakiwa wamevaa vazi hili wakiwa si wanene sana wana umbo la kawaida, lakini si mtu uwe mnene sana halafu unavaa vazi hili cha kuzingatia kwanza angalia umbo lako je litafaa kwenye vazi hili.
Na hili ni moja wapo ya mtindo wa vazi la kitenge linalo pendeza sana, unaweza kushona mitindo mbali mbali ya kitenge ikiwemo kushona kaptura kama unavyo apo juu kwenye picha.
0 comments:
Post a Comment